Tuesday, September 19, 2017

MAOMBI KWA TUNDU LISSU.


Related image


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Moshi kiko kwenye hatua za mwisho za kuandaa kongamano kubwa litakalo enda sambamba na maombi maalumu kwa ajili ya Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU anayepatiwa matibabu nchini Kenya baada ya kupigwa risasi hivi karibuni.
Katibu wa Chadema wilaya ya Moshi EMMANUEL MLACK aliyasema hayo katika kikao na waandishi wa habari wakati wakitoa taarifa ya kulaani kupigwa risasi kwa LISSU huku wakitangaza kuunga mkono azimio la kamati kuu ya Chama hicho la kutaka wachunguzi wa maswala ya jinai kutoka nje ya nchi.
Alisema CHADEMA Moshi vijijini ina laani kitendo cha kuzuiliwa kwa wananchi kufanya maombi kwa ajili ya LISSU apate kupona huku akilitaka jeshi la Polisi kutumia busara kipindi hiki kwani kinachofanyika ni masuala ya kiimani.
Kuhusu Kongamano hilo MLACK alisema mbali na shughuli nyingine pia wanakusudia kuitumia siku hiyo katika kuchangia damu kutokana na kuwepo kwa hitaji kubwa la Damu kwa wagonjwa katika Hospitali zetu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA ) jimbo la Vunjo BONIFACE MBANDO alisema hoja ya Chadema si pekee ya kupigwa risasi kwa LISSU bali ni mrundikano wa matukio mabaya yenye mlengo wa kisiasa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kimochi ELIFAMIA MASAMU amesema tukio la kushambuliwa kwa LISSU ni la kinyama hasa kwa mtu ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za wanyonge bila kujali Kabila, Dini, Ukanda na Itikadi za kisiasa.

No comments:

Post a Comment

Polisi 6 wakamatwa kufuatia kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwiline Tanzania

Maafisa sita wa polisi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanafunzi wa chuo cha kitaifa cha usafirishaji Akwilina Akweline. Hayo ni k...